Tofauti kati ya mfanyabiashara na mjasiriamali (Jitambue)


  1. Tofauti kati ya ujasiriamali na ufanyabiashara

Ujasiriamali unaweza kuipata maana yake halisi kwenye
Jina lenyewe ujasiriamali ( ujasiri kwenye mali) hivyo ili
Kuwa mjasiriamali lazima uwe jasili na  mwenye uwezo
Wa kukubali matatizo na changamoto, uwe tayari kupoteza
Sasa hivi kwa ajili ya mafanikio ya baadae.

Ukiwa mjasiriamali faida za muda mfupi kwako huwa sio za muhimu sana na lengo
Kubwa huwa ni kufikia malengo uliyoyapanga na kukamilisha ulichokifikiria
Watu wengi hujiona ni wajasiriamali kwa vile tu huwa na uwezo wa kutatua matatizo
Ya biashara yake kwa kutumia njia nyingine .

Mfano: utakuta mtu anafanya kazi ameamua kuanzisha biashara yake pembeni ya kazi
Anayoifanya ambapo inafikia hatua anapata hasara au bashara hailipi kwa muda husika
Anachoamua kufanya ni anachukua fedha kutoka sehemu anakofanyia kazi anaziba pengo
Lililopo kisha anaendelea na biashara, huyu anaweza kujiona ni mjasiriamali lakini sio
Huyu ni mfanyabiashara .

Unapokuwa mjasiriamali ikitokea kuna kitu kimegoma au mambo hayaendi kwa mjasiriamali
Huwa hakuna njia za pembeni ila ndani ya tatizo huwa kuna suluhisho mfano: umeamua kuwa
Mjasiriamali mkulima umelima na umevuna sasa imefikia kipindi cha kwenda kuuza na hauna
Fedha za kusafirisha mazao yako, unaweza kwenda kwa watu wanaohusika na usafirishaji  wa
Mazao na kufanya nao makubaliano kwa aidha ukimaliza kuuza uwalipe au wachukue kiasi fulani
Cha mazao yale.

Tofuti iliyopo kati ya mfano wa kwanza na wa pili ni kwamba  wa kwanza ametumia fedha nyingine
Kumaliza tatizo la sehemu nyingine hivyo kwake hawezi kujua ugumu na jinsi ya kutatua matatizo
Zaidi ni itakuwa anajua namna ya kumaliza tatizo kwa  kutumia sehemu nyingine lakini wa pili
Ametumia kile kile anachokiamini kinamletea faida na anauhakika nacho kutatua matatizo
Ya muendelezo wake.


Mfanyabiashara ni yule ambae anatafuta faida ya kile anachokifanya kwa muda ule ule
Anapotoa anauza anahitaji apate faida aendelee na biashara yake ila hayuko tayari kupokea
Hasara na yeye hayuko tayari kupokea hasara, iwapo itatokea ni rahisi kwa yeye kubadilisha
Biashara ilimradi iwe inafaida tu.


lengo kuu  ya biashara ni kuuza na kununua kukiwa na faida ndani
Yake ambapo faida kidogo inabaki  yako na nyingine unaongezea kwenye
Mtaji. Lakini ujasiria mali lengo kuu lake ni kufanya unalofanya  kwa manufaa ya  baadae
Na ukiwa na uaminifu wa asilimia kubwa kwa unachokifanya hata kama haikupi
Faida kwa muda huo.


Nafikiri ifike hatua sasa watu wajitambue na pia watembelee njia zinzoendana na asili yao, jitambue
Ni mjasiriamali au mfanyabishara ili uwe kama asili yako inavyotaka uwe ukiwa mfanya biashara ukajilazimisha
Kuwa mjasiriamali ni lazima utafeli na ukiwa mjasiriamali ukijilazimisha kuwa mfanyabiashara hautafanikiwa .

Comments

  1. Ashante kwa ufafanuzi, sasa nimeelewa maana ya mfanyabiashara na mjasiriamali

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango