Maswali 12 kuhusu Branding

Maswali ya Msingi unayotakiwa kuyafahamu kabla ya kuanza kubrand.

1. Brand ni nini?
Brand kwa maana moja tunaweza kusema ni muonekano wa biashara yako, branding ni
muonekano wako Kuhusu biashara yako na jinsi gani biashara yako inajitofautisha na
washindani wenzako,

2. Kazi za Brand.
  1. Brand hutambulisha muonekano ,ubora wa kuaminika kwa watu, huku bidhaa za generic(kawaida) hazijulikani na haziaminiki ,hata hivyo brand ni ghali na inahitaji mipango ya muda mrefu.
  2. Brand hutofautisha bidhaa na hufanya bidhaa kutambulika mapema
  3. Brand inaruhusu mtumiaji kutengeneza maamuzi na matumizi ya bidhaa
  4. Brand hutengeneza thamani halisi kwenye macho ya washirika wa kibiashara na hupenyeza thamani ndani ya macho ya mtumiaji.
  5. Branding hutengeneza trademark ambayo huongeza thamani ya bidhaa.
3. Kwanini ufanye brand

    Unafanya brand kwa sababu unataka kutambulika na kuongeza mauzo , pia ni kutaka
    kujitofautisha na washindani wako

4. Faida gani unayoipata ukibrand
     Brand hukutambulisha
     Brand hukutofautisha,
     brand hutengeneza thamani,
     Brand hukutengenezea trademark

5. Hasara za kutokubrand

Hautajulikana kwenye soko,mauzo yako hayataongezeka,hautapata nafasi kwenye ushindani

6. Mifano ya Brand zilizofanikiwa
   
                       a. Steps entertainment (usambazaji muvi)
                       b. Msama promotion (matamasha- dini)
                       c. Cocacola(Vinywaji)

Mifano Brand zilizofeli

                        a. General tyre(Michellin)
                        b. Yebo yebo (kinywaji)

7. Brand inasimamiwa na vitu gani?
                a. Nembo
                b. Brand
                c. Utambulisho
                d. kutokubadilika

8. Mgawanyiko wa Brand
             a. Brand ya mtu
             b. Brand ya Kampuni/mfumo
             c. Brand ya Bidhaa
             d. Brand ya Alama

9. Nianze kufanya nini?
             Tengeneza Alama , halafu jibrand uje utengeneze mfumo then bidhaa

10. Tofauti kati ya kampuni na Brand
       Kampuni ni jina la wamiliki wa Brand
        Na Brand ni ahadi unayotaka kuiweka kwa wateja wako, ( ahadi ya mmiliki kwa mteja)
        Kutafuta Masoko - ni kujenga brand kwenye akili ya mteja unaemtegemea

11. Tofauti kati ya elimu ya ujasiriamali na branding

Elimu ya ujasiriamali- ni elimu inayotolewa kwa ajili ya kukutengenezea njia za kujiajiri na
                                        kujiongezea mapato.
Elimu ya Branding - Ni elimu ya kujua njia na jinsi ya kuongeza mapato na kujulikana kwenye
                                    kipengele chako cha ushindani

Makampuni mengi na watu wengi hushindwa kusimamia brand zaokwa vile tu hukosa elimu
sahihi ya kubrand, branding ni elimu ambayo utaitumia kila sehemu kwa sababu inaanzia kwa
mtu mmoja mmoja hadi kampuni.

Kuongezeka au kupungua kwa masoko sio kazi ya masoko bali ni kazi ya branding

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango