Vitu vya kutambua kabla ya kuwa mfanyabiashara au mjasiriamali

Vitu  vya kutambua kabla  ya kuwa mfanyabiashara au mjasiriamali  

Ujasiriamali  imekuwa ni ndoto ya watu wengi sasa hivi, kila anaepata nafasi au wazo la biashara
huanza kujiita mjasiriamali lakini kuna maana na mambo mengi ambayo mtu anatakiwa ayajue kabla ya kuanza biashara na anatakiwa achague kati ya ujasiriamali au ufanyabiashara.

leo nitaelezea mambo kadhaa ambayo unatakiwa kuyafahamu kabla ya kuwa aidha mjasiriamali au mfanyabiashara na baadhi ni mambo ya kawaida na tunakutana nayo kwenye maisha yetu ya kila siku lakini ni sawa na ukiona sululu bila kuambiwa ni sululu na inafanya kazi gani utakuwa unaona iko kama uma lakini unaweza kupatia  au kukosea matumizi yake kwa kuiona tu, vivyo hivyo hata kwenye ujasiriamali pia kuna vitu ambavyo unatakiwa kuvifahamu.unaweza kuvifanya bila kuambiwa na ukawa sawa ila ukiambiwa utaweza kujiamini na unachokifanya zaidi ya mwanzo.

Kabla ya kuanza biashara

1. Kukubaliana na hali  
 
Katika vitu  vikubwa ambavyo wafanyabiashara hukumbana navyo na kuwa kikwazo ni kukubaliana na hali ,utakuta mtu anaona eneo alilopo au biashara anayotaka kufanya hana uzoefu nayo ila kwa sababu ya shinikizo na kutamanishwa faida anaanzisha biashara hiyo mwisho inamshinda.

Kukubaliana na hali ni jambo la msingi sana ili biashara yako ifanikiwe ni lazima ukubaliane na hali yako ya uelewa, uchumi,eneo, biashara yenyewe invyotaka. tofauti na hapo biashara yako itakuwa ni ngumu sababu aidha itakuwa inahitaji vitu tofauti na ulivyo navyo au itakuwa inakinzana na wewe mwenyewe.

2. Kutegemea kufeli sio kushinda tu

katika biashara ni lazima kuna baadhi ya mambo lazima utafeli tu hata kama umejipanga na una misingi mizuri kiasi gani hivyo kabla ya kuanza biashara unatakiwa ujue pia ndani yake sio kushinda tu kuna siku ambazo hasara itakuja kwako  na utaipokea hata kama hutaki.

 3. Kuyaruhusu matatizo yaje

kuna usemi mmoja unasema matajiri huomba matatizo yawatokee ili waweze kuyatatua, lakini masikini huomba matatizo yasije ili yasimpate. Matatizo mimi ninavyoamini kila kitu kina matatizo hata mawe pia yana matatizo yake lakini kwa vile hayana mdomo wa kuelezea,hivyo matatizo ni lazima yaje na hasa kipindi unapoanza kabla haujajiimarisha,kipindi hiki huwa kina matatizo  sana na kuna wengine hukata tamaa sababu ya wingi wa matatizo, lakini MATATIZO NI CHANGAMOTO,usichukulie tatizo lako ni kama kikwazo ligeuze liwe changamoto utaona  njia za kulipunguza na hata kulimaliza ila ukifanya changamoto kuwa tatizo basi ni ngumu kulikubali na kulitafutia ufumbuzi.


4. Kuwa na msimamo na unachotaka kufanya
Kabla ya kuamua kuanza biashara hakikisha unamsimamo na kitu unachokileta katika soko, watu wengi wamekuwa wanafanya biashara kwa majaribio utaona leo anatambulisha kile  baada ya muda mfupi anatambulisha biashara nyingine hapo ukifanya hivyo biashara yako haitakua, hivyo ni vizuri kuleta kwenye soko wazo na biashara ambayo unaiamini kwa kiasi kikubwa na unaweza kudumu nayo.

  5. Kuyapima mambo kabla ya kufanya

Watu wengi wamekuwa wanafanya mambo bila kuyapima kwa kuwa wanahisi waliowaambia hawawezi kukosea , hilo ni kosa kubwa kama mfanyabiashara unatakiwa uwe na uwezo wa kupima kipi nifanye na kipi nisifanye tofauti na hapo utajikuta unafanya mengi yasiyokuwa na faida kwako,hakuna mtu anaepatia muda wote hata mashine zilizotengenezwa kupatia tu hukosea ( ATM,Simu,kompyuta) sembuse mwanadamu anaefanya kila kitu kama wewe ila tofauti ni uwezo wa kufikiri na kufanya kazi, hivyo sikiliza yote ila usifanye yote pima na chuja ni kipi kina kufaa.

6. Kuwa na plan b

Kama mfanyabiashara unapoingiza biashara yako sokoni unatakiwa uwe na plan B ya biashara yako kwa kuangalia ushindani upenyo na kipi kinahitajika hii inamaana kuwa iwapo utakuwa na plan B hata kama plan A ya biashara ikiyumba au kutokufanikiwa unaweza kutoa plan b, hapa haimaanishi kubadilisha biashara ni kubadilisha plan mfano biashara yako inaweza ikawa ni ya kuuza magari kwa kuyaleta na kuyauza bila kuangalia mteja au kuna mtu analihitaji lakini baada ya muda biashara hiyo inaonekana haitoki  sababu watu hawanunui gari zilizopo plan B inaweza kuwa ni unabadilisha mtindo wa uuzaji sasa ni unaanza kuleta gari kwa oda maalum mteja kaja kwenye eneo lako la biashara kaangalia kakosa gari anayoitaka unamwambia akupe oda kwa kiasi kadhaa baada ya muda flani gari yake ataipata au unaanza kufanya mteja anatoa oda kwenye mtandao halafu wewe utaifatilia, hiyo ndio plan B ninayomaanisha ni muhimu pia kuwa nayo kabla haujaanza biashara.

  7. Usifanye biashara kwa kujaribu

Kabla ya kuingia kwenye biashara jiulize kwanza kama uko tayari na haubabaishi, katika dunia hii ya utandawazi kila kitu kipo ila vinvyokuja ni marekebisho na muedelezo wake tu, hivyo biashara ambayo unataka kuifanya wewe iangalie sana usiifanye kwa kujaribu kwa sababu kuna wengine hawaijaribu ambao ndio washindani wako, utapoteza nguvu zako bure kama bado haujawa tayari kuanza biashara acha usijaribu itakuumiza.

hayo ni baadhi ya mambo muhimu unayotakiwa kuyajua kabla ya kuwa mfanyabiashara au mjasiriamali  toleo lijalo nitaelezea baadhi ya mambo muhimu unayotakiwa kufanya   baada ya kuanza biashara au ujasiriamali

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango