Tofauti kati ya Branding na Marketing ( Masoko)


Kumekuwa na Mkanganyiko wa matumizi pia ya hivi vitu viwili Branding na Marketing ( Masoko) na imekuwa ni tatizo kugundulika ipi inayotakiwa ianze kati na ipi ni kubwa zaidi ya mwenzake .
kwa upande wa Branding tayari nilikwisha elezea kwenye toleo za nyuma Branding.

Leo nitaelezea kidogo maana ya masoko na tofauti yake na Branding

Masoko (Marketing)  ni kila mkutaniko wa kampuni yako na mtu au kitu chochote duniani

Maana ya marketing ( Masoko) inajumuisha; Jina la biashara,mgawanyo wa aidha unatoa huduma au bidhaa,njia za utengenezaji au utoaji huduma,rangi,saizi na umbo la bidhaa yako,upakiaji,eneo la biashara,kujitangaza,mahusiano na jamii, tovuti,Branding,email,sahihi yako kwenye majarida na chochote unachokitoa ,ujumbe wa sauti,matamasha ya mauzo,simu,mafunzo ya uuzaji,jinsi ya kutatua matatizo, mipango endelevu ,watu wanaokuwakilisha,wewe,unavyofuatilia

Lakini pia kwa upande mwingine marketing(Masoko) inajumuisha,wazo kuu la brand yako,huduma yako,muelekeo wako na upendo unaouleta( kuuonyesha) kupitia biashara yako.Kama ukiyakusanya yote kwa pamoja basi biashara yako itafanaikiwa.

Marketing ni sanaa ya kuwakusanya watu ili kuwabadilisha mawazo yao

Muda wako mwingi wa marketing ni vizuri ukiutumia kwa wateja ambao tayari unawafanyia kazi.

Marketing pia ni ukweli unaovutia

Marketing ni maumivu ya taratibu ambayo yanahamisha watu kutoka sehemu zao walizozoea na kuhamia kwenye list ya wateja wako,kwa uangalifu  huchukua na kufumbata  ndani ya vichwa vyao na usiruhusu itoke, kila  kitu  kinachosaidia wewe kuuza bidhaa au huduma hicho ni sehemu ya taratibu za marketing.

hiyo ndio maana halisi ya marketing ( Masoko) lakini branding maana yake ni alama au muonekano wako kwa mteja wako na mteja unaemtarajia kwa maelezo ya haraka haraka tukiangalia marketing ( masoko) ni zao la Brand,kwasababu ili ufanye marketing ni lazima uwe na brand unapoenda kumfata mteja au mteja mtarajiwa zoezi unalolifanya ni kumhamishia brand yako toka kichwani kwako hadi kwake 

Mfano: Unakutana na mtu anatembea labda amebeba mfuko haujui ndani yake kuna nini, unapokutana nae kitu cha kwanza ni atakusalimia halafu atakupa brand yake '' naitwa Mussa natokea kampuni inaitwa Don, kampuni yetu inajishughulisha na kuuza bidhaa/ kutoa huduma zifuatazo..." 

Katika huo mfano mfupi kitu cha kwanza alichokifanya Bw. Mussa alitoa brand yake kwa maana ya jina halafu kitu cha pili akatoa na brand inayomfadhili kwa maana ya Don halafu kitu cha tatu akataja brand za huduma au bidhaa zinazotolewa kutoka kwa mfadhili wake na mwisho atamalizia na kuanza kuzifanyia masoko kwa kuzisifia na kuziongezea ubora na upenzi kwa msikilizaji ,masoko ni kazi ya kuhamisha brand kutoka kichwani kwako kwenda kwa mtu mwingine.

Brand na masoko ni vitu ambavyo vinaendana sana lakini cha kwanza kati ya hivyo ni  Brabding unatakiwa ufanye branding ya bidhaa/huduma yako kabla ya kuanza kutafuta masoko, kwa sababu usipoifanyia branding biashara yako unaweza hata usionekane katika soko.mauzo ya bidhaa au huduma hayategemei sana ubora wa kitu bali ni kiasi gani umeibrand biashara yako.

 Mfano: Ukiingia ndani ya jengo Mlimani city mall kurudufu nakala bei yake ni shilingi 500 hadi 1000 inategemea na sehemu lakini ukitoka nje ya jengo hilo bei ya kufanya huduma hiyo ni shilingi 50 hadi 100 lakini wateja wengi ni wale ambao wanaenda kupata huduma kwenye bei ya 500 hadi 1000, Kwanini ? hii ni kwa sababu ya Brand ya jengo lenyewe jengo ndio ambalo limetoa thamani na muongozo wa biashara hata kama akija mwingine akisema yeye kufanya huduma ile ile ni 2000 bado atapata wateja lakini hiyo ni kwa sababu tu yuko ndani ya jengo.

Mfano 2: Kwa wapishi waliozoea kununua unga labda wa mahindi/ngano/mhogo au unga wowote unaotumika katika mapishi ikitokea ule unga ukawa umeharibika lakini amekwisha nunua,akienda kuutumia asipopata matokeo chanya hawezi kuelekeza lawama au tatizo kwenye unga kwanza atafikiria labda ni nishati imepungua au kuongezeka sana au labda ni uzembe wangu leo na mawazo mengine kama lakini kila akifikiria unga anakuwa anajiambia mwenyewe" haiwezekani wale watengeneze  kitu kimeharibika" 

Mifano yote miwili inaonyesha nguvu ya branding na masoko na kipi kinachotakiwa kuanza katika mfano wa kwanza mjenzi ndie aliefanya brand ya jengo kwa hadhi yake,halafu anaekuja kuchukua nafasi anajitengenezea soko kupitia brand ya jengo na kwa mfano wa pili kutokana na brand iliyofanyika mwanzo ya unga huo tayari mtumiaji huyu kichwani kwake kuna ubora wa unga kwa maneno lakini sio vitendo ambapo brand imemuaminisha kwa kiasi kikubwa kwamba unga ni bora kwa pishi atakalohitaji kutumia hivyo hata kama unga sio bora tayari brand imeshampa picha ya ubora wa unga ambao hajauona ,hivyo brand ni ya muhimu sana.

Kabla ya kuanza kufanya marketing (kutafuta masoko) unatakiwa uanze kwanza na kubrand sababu brand ndio msingi ndio picha ya bidhaa au huduma na masoko ni kazi ya kuichukua picha ile na kuipeleka kwa mteja.


Karibu katika semina ya Mafanikio inayoendelea semina hii ni nchi nzima karibu (mawasiliano 0684047323)

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango