Ukweli kuhusu ujasiriamali
Nimeshaandika sana
kuhusiana na ujasiriamali japo sijafikia sehemu ambayo inatakiwa lakini
inatakiwa tufikie hatua tuache kudanganyana kuwa mjasiriamali sio suala
dogo lakini watu wamefanya kama vile ni
kitu ambacho kila mtu anaweza kukifanya, ujasiriamali sasa umekuwa ni wimbo
kila mtu ni mjasiriamali hata muuza vitumbua nae ni mjasiriamali tunapoteza
vijana wengi kwa wadanganya kuhusiana na ujasiriamali , ukweli ujasiriamali ni
mgumu na tena sio mgumu kidogo ni mgumu sana.
Ukianza kiuangalia
nadharia ya ujasiriamali ni mtu mwenye
ujasiri na nguvu kwenye mali lakini tofauti na ambavyo tunauangalia kwa upande
mwingine ambavyo ndivyo asilimia kubwa wanafahamu kwamba ujasiriamali ni uwezo wa kufanya au kumiliki biashara yako , huo
ni uongo tena mkubwa, tunakopi vitu kutoka nchi zilizoendelea halafu tunatafsiri
vibaya , ukiangalia watu wanaoitwa wajasiriamali kwa nchi za nje ni tofauti
kabisa na wanaoitwa wajasiriamali wa huku, na kitu kibaya zaidi ni kwamba
tunakopi mifano ya kuvutia (Inspiration) kutoka kwao lakini hatufanyi kama
wao,taifa tunalolitengeneza sio
tunaloliombea , tunajitahidi kila siku kuwa tuna washawishi vijana wetu kufanya
ujasiriamali wa kujiajiri mwenyewe , hata hapo pia haiwezekani hakuna
mjasiriamali aliefanikiwa kwa kufanya ya kwake
peke yake wote ambao ndio mifano yako ya mvuto fuatilia ni lazima
aliajiriwa kwanza au alianza kwenye sehemu ya mwingine halafu baadae ndio anaanza kuja kufanya sehemu yake
, hivyo usije ukadanganywa eti ukitaka
kufanikiwa inabidi ujiajiri mwenyewe kwanza
ni lazima uajiriwe kwanza au upate ujuzi wa hiyo kazi ndio uanze
kujiajiri, na ujuzi unaopewa katika ngazi za elimu zetu ni wa kusaidia kompyuta kukamilisha kazi yake, hivyo kuajiriwa ni lazima kabla ya kuanza kutembelea ndoto yako, hasa kwa nchi ambazo zinaendelea kwa sababu uwezo wa kutengeneza na kuvumbua umedidimizwa na vitabu vya wavumbuzi wengine wa zamani.
Ujasiriamali ni kitu
ambacho unatakiwa kutulia sio kukurupuka
nacho ni lazima ujifunze kuwa na subira na usifanye ujasiriamali kama mpango
wako ni kupata fedha peke yake kwa sababu
unapokuwa mjasiriamali ni lazima ufanye
biashara kwa matokeo ya baadae mjasiriamali hafanyikitu kwa ajili ya faida au matokeo ya muda mfupi ndio maana
asilimia kubwa ya mifano ya watu tunaowaona kama mifano katika maisha ya
ujasiriamali hawakuanzia kwenye mafanikio ila wameanzia kwenye hali ya kawaida
sana na ya chini lakini mafanikio yao yamekuja baada ya muda mrefu tofauti na
sisi ambao mawazo ya ujasiriamali tunapewa halafu bado tunataka tufanikiwe
ndani ya kipindi kifupi, wote waliofanikiwa na kuwa wajasiriamali mifano
walikuwa wanaishia ndoto zao kuna ambao kutokana na kuyaamini mawazo yao na
kuyakubali kwa kiasi kikubwa iliwagharimu hata elimu zao kuna walioacha masomo
sababu ya kufatilia ndoto zao,wapo walioacha kazi na hata familia lakini
tofauti na kwetu unakuta mtu hajajiandaa
hata kuwa na hiyo ndoto unatembea na ndoto mbili au ndoto zaidi ya nne na bado
hata haujakamilisha moja unapewa ndoto nyingine ili ukamilishe ndoto yako mpya,
ukweli ni kwamba hapo utakuwa unatumikia ndoto ya mtu mwingine huku unazika za
kwako na huwezi kufanikiwa pia ukiwa na ndoto zaidi ya moja ifikie hatua watu
wajitambue ndoto ni moja na hiyo ndio
itakayo kupa mafanikio yako , tunatengeneza taifa ambalo litakuja kuwa zaidi ya
tegemezi sababu baada ya muda hao
tunaowaita wajasiriamali hawatakuwa na uwezo wa kusimamia tena biashara zao na
wataanza kutafuta misaada watakaokuwa na pesa kwa kipindi hicho watakuwa ni
wale waliokomaofisini na wafanyabiashara hivyo pesa itakuwa mikononi mwa watu
wachache na hao watawaburuza hao wanaojiita wajasiriamali.
Kuna mengi ya kuamua
kabla ya kuwa mjasiriamali tusikurupuke na kuanza kujiita tu wajasiriamali
jiulize kwa maelezo hayo hapo juu wewe ni mjasiriamali au mfanyabiashara , na
gundua ndoto yako mapema na uifanyie kazi sio kukaa pembeni na kusubiri elimu
ikuamulie kazi yako, soma unachokitaka sio fedha inachokitaka unatakiwa kujua
kuwa fedha ni matokeo ya huduma hivyo jifunze huduma ambayo itakupa furaha na
faraja hata bila ya kupata pesa kama tokeo la mwisho ujasiriamali sio kitu
kidogo yafaa kuelewa maana kwanza na sio kufanya kwa mkumbo unaweza kupoteza
muda na fedha zako bure.tuache kutengeneza tafsiri nyepesi ya maneno magumu.
Fuatilia masomo
ujasiriamali na biashara kupitia semina ya MAFANIKIO maelezo zaidi yako kwenye
matoleo ya nyuma na ukurasa wa
matangazo.
Comments
Post a Comment