Vitu 10 (Kumi) vitakavyofanya biashara yako ifanikiwe

Bishara yako haiwezi kujiendesha yenyewe bial kuwa na vitu vinavyoisimamia leo nimekuletea vitu 10 vitakavyoifanya biashara yako ifanikiwe, ni vitu ambavyo tunaviona ni vidogo na vipo katika maisha yetu ya kila siku hivyo tunavifanyia mazoea lakini sasa

1. Ipende biashara yako.

Biashara yako ni maisha yako ndio mfereji wa kipato chako hivyo inatakiwa ipendwe na kuthaminiwa,unapoweka upendo wa kutosha kwenye biashara yako lazima mafanikio yatakuja yatakayokuja, fanya biashara kwa upendo na moyo wa kujituma.usifanye biashara yako kama ya jirani yako ipende na ithamini itakupenda na itakulipa.






2. Jenga uamninifu.

Katika biashara kitu cha muhimu kuliko yote ni uaminifu sababu mteja anapokuja kununua au kupokea huduma kutoka kwako ni kutokana na uaminifu kwako na kuamini huduma yako hivyo  fanya kazi kwa uaminifu sikuzote kwa mafanikio na maendeleo ya biashara yako.Uaminifu wako ndio mafanikio yako fanya kila kitu kwa uamnifu .








3.  Usibadilike badilike.

Moja kati ya vitu vinavyoondoa uaminifu na muonekano wako mbele ya wateja wako ni kubadilika badilika leo unafanya biashara hii kesho biashara  ile unaua maendeleo ya biashara yako,kutokubadilika ni siri ya mafanikio ya biashara nyingi, watu wengi huwa wanachanganya kati ya kutengeneza sub-brand na kubadili biashara. Mfano watengenezaji wa bia ya Castle lager walipoleta Castle lite sio kwamba walibadilisha biashara bali walileta sub brand( brand saidizi) ni tofauti iwapo Castle lager wangeamua kuleta kinywaji kingine chenye jina tofauti na Castle huku watengenezaji wakiwa ni wao wenyewe hapo ingekuwa wamebadilisha brand (muonekano,picha ya biashara),usibadilike badilike kwa kufata upepo wa pesa toa huduma au bidhaa pesa iwe ni matokeo ya huduma au bidhaa.


4. Usiruhusu uoga /kushindwa kukakurudisha nyuma

Biashara ni mashindano na katika mashindano nia kuu ni kushinda hata kama mpinzani wako unamfahamu anauwezo kiasi gani matarajio ni kushinda, pia hata katika biashara ni hivyo hivyo nia kuu ni mafanikio na biashara kukua hata utakutana na vikwazo kiasi gani hautakiwi kushindwa ,pesa ni mchezo wa kunyang'anyana wewe unapokuwa nayo ni mali ya mwingine na mwingine anapokuwa nayo ni mali yako, iwapo utakuwa muoga  au ukikubali kushindwa utakuwa unapokea tu mali ya wengine bila wewe kuchukua ya kwako.Usikubali kurudishwa nyuma changamoto ndio biashara. Uoga wako utakupotezea  mafaniko yako iwapo utauruhusu

5. Fanya maamuzi kwa kuendana muda.

Hapa pia kuna tatizo kubwa kwa upande wa hapa kwetu maamuzi yetu hayaendani na muda ila yanaendana na mawazo yetu, muda nnausemea hapa sio ule wa dakika ama saa ila muda kwa maana ya maamuzi ya kibiashara kulingana na hali ya soko, asilimia kubwa ya wafanyabiashara wanandoto za kufanikiwa kuwa kama watu wanaowatamani kutokea nje ya nchi na wengine ndani ya nchi pamoja na kuwa hivyo lakini tatizo linakuwa unatamani kuwa kama yeye lakini haufanyi kama yeye.hapo haitawezekana itakuwa sawa na serikali ilipoamua kupunguza wimbi la ajira kwa vijana kwa kuruhusu ujasiliamali wa vitu vidogo vidogo  lakini baada ya muda ikangundua dunia inatumia barcode na hawapati kodi sasa wameamua kuanzisha utaratibu wa ili bidhaa yako iwe sokoni  ni lazima ipitie TBS na TPDF kwa ajili ya kuhakikishwa kwanza hii ni kufanya maamuzi ya mwanzo bila kuendana na wakati Barcode na shirika la viwango yapo toka zamani na matumizi yake yanajulikana tangu zamani lakini sasa madhara yanakuja kwa mjasiriamali mdogo ambae hawezi tena kufatilia na kufuata taratibu zote mwisho ni kwamba unamrudisha alikokuwa mwanzo. Tumia muda na maamuzi yako kwa kuendana na soko lako na matokeo ya baadae usifanye kwa ajili ya leo na kesho kuna kesho kutwa ambayo hauwezi kuirudisha.

 

6. Kumbuka wewe ni mhimili mkubwa katika biashara.

Japo biashara yako sio ewe lakini ukweli ni kwamba biashara ni wewe mwenyewe unatakiwa kutambua kuwa  inakutegemea wewe mwenyewe ili iweze kukuletea faida ,muonekano wako, majibu yako, maamuzi yako, mavazi yako yanamatokeo ya moja kwa moja kwa mteja na biashara yako hivyo unatakiwa ujitambue na uione nafasi yako katika biashara yako .
mafanikio au kufeli kwa biashara ni kutokana na maamuzi yako wewe ndio mhimili wake , Biashara yako





7. Simamia vizuri wivu wako.

Katika biashara napo kunatakiwa wivu na hakuna mtu asiekuwa na wivu lakini hapa unachokumbushwa tu ni kuusimamia vizuri wivu wako, wivu wa biashara ni ule wivu ambao unamuona mfanyabiashara au mjasiriamali mwenzako amepata mafanikio na wewe unapata wivu wa hamu ya kuwa vile,lakini hiyo hamu unayoipata ndio inatakiwa iwe na kiasi mfano; wewe unauza nafaka na mwenzako pia anauza nafaka mwenzako akaanza kutafuta masoko akapata wateja wengi akaongeza mtaji wewe bila kugundua kiini cha mafanikio na wewe ukachukua mtaji na faida vyote ukaviweka ili biashara yako ilingane na biashara yake hapo utakuwa umepotea kwa sababu kesho na kesho kutwa ukipata tatizo hautaweza kulimudu sababu malengo yako yamehamishwa na sasa unakuwa mtumwa wa mafanikio ya mtu mwingine. Usimamie wivu wako uwe na kiasi na ujifunze kufatilia mambo kwa undani.

8. Sifia na kubali kukosolewa.
Kuna watu ukiwakosoa ni kama umetenda kosa la jinai , mara zote wao hujiona wanajua kila kitu na wanaweza kufanya kila kitu lakini ukweli ni kwamba anaejiona anajua kila kitu huyo ni mjinga, na mjinga akifeli hujiona anaweza  sana kwa sabau hutengeneza njia za kujilinda na kufeli kwake, hivyo ili biashara yako ifanikiwe kubali kusifia kuanzia unaofanya nao kazi hadi washindani wako, biashara sio sehemu ya kusambaziana chuki na uhasama wote ni binadamu na tuliumbwa na upendo hata kama ni mshindani wako akifanikiwa msifie  na wewe pia kubali kukosolewa  hauwezi ukafanya kila kitu sawa sawa hata kama unakijua  asilimia 100, kuna aina nyingi mno za makosa ya kiufundi, binafsi, ya mitambo n.k hivyo ukikosolewa ni njia mojawapo ya kupewa mbinu ya kufanikiwa kwa sababu biashara ni mchezo wa kutumia makosa ya mwenzako.

 

9. Simamia kufanya kazi kwa bidii na umoja.

Siku zote katika biashara yako himiza na simamia ufanyaji kazi kwa bidii na kwa umoja iwapo ofisi ikifanya kazi kwa bidii na umoja mafanikio yake yataonekana mapema  ila kama ufanyaji kazi utatawaliwa na chuki pamoja na visasi hakutakuwa na mafanikio yanayotarajiwa, yafaa turudi tulikotoka "utu kwanza pesa baadae" na umoja  ni msingi wa mafanikio simamia hapo na matokeo yake yatakuja hivi karibuni.




10. Kuwa na Imani.

Kila mtu anaimani na kitu anachokiamini hivyo weka imani yako pia katika biashara yako hata kama matokeo  nafaka ni sawia kesho unaamini kuuza magari ndio sawia hapo hautafanikiwa biashara ni ile ile kila sehemu kuna changamoto zake amka sasa iamini biashara yako na ipe hadhi ya imani yako utafanikiwa.
yake sio mazuri kwa kipindi kirefu angalia tatizo ni nini na iamini ndio biashara itakayokupa mafanikio na kukufikisha katika ndoto zako usiifanye kwa kujaribu fanya kwa nia na imani ya juu,usichanganye imani katika biashara moja leo unaamini kuuza

Hivyo ndivyo vitu 10 vitakavyofanya biashara yako ifanikiwe na ikue hadi mahala unapopahitaji hakuna miujiza katika biashara na hakuna mazingaombwe katika biashara  ni kutambua yanayokufaa  na kuyafanyia kazi kwa moyo na ari ya kutaka kuyatimiza, mafanikio yako kwa kila mtu "umezaliwa ili ufanikiwe sio ufeli" tumia mbinu hizo na utafanikiwa.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango